ZINC MADINI YANAYO PONYA MAGONJWA YA MWILI

Unapotumia Virutubisho (Supplements) tumia kwa mujibu wa Ushauri wa daktari. Haina maana kama sio dawa za Kemikali basi kila mtu anaweza kushauri utumie Virutubisho dozi na Uhusiano wa madini au vitamins zingine Kuna umuhimu wa kujua.
.
Huwa nakutana na wagonjwa wengi tu wanatumia supplements bila kuwapa msaada badala yake zinaongeza matatizo.
.
Mwili wa binadamu unakisiwa kuwa na gramu 2-4 za madini ya zinc. Na hupungua kila siku kwa asilimia 0.1. Madini ya zinc hutumika mwilini bila kuisha nguvu kwa siku 280. Asilimia 57 ya zinc huwa ipo kwenye misuli na asilimia 29 ipo kwenye mifupa. Mwili huwa hauna sehemu na mfumo wa kuhifadhi madini haya. Hivyo tunalazimika kupata madini haya kila siku kwenye vyakula tunavyokula.
Kwa siku unashauriwa upate madini ya Zinc miligramu 11 kwa mwanaume na miligramu 8-9 kwa mwanamke.
.
Kama unatumia Virutubisho na Unatumia dozi zaidi ya 40mg kwa siku hairuhusiwi kuendelea na dozi hio kwa zaidi ya wiki 2. Na kama unatumia dozi zaidi ya 40mg kwa siku kwa muda mrefu Inashauriwa utumie sambamba na madini ya Copper. La sivyo utapungukiwa madini ya copper mwilini na Kuibua magonjwa mengine.
.
Inashauriwa kama unatumia zinc utumie chini ya uangalizi wa daktari ili aweze kukupa dozi kulingana na Tatizo lako na Atachukua tahadhali kulingana na Tatizo lako.
.
Zinc: Madini yanayo Ponya mwili.
1. Kujenga mwili
2. Ukuaji wa mwili
3. Kukinga mwili dhidi ya sumu za Vyakula
4. Kuponyesha majeraha haraka
5. Kuongeza kinga ya mwili
6. Husaidia utengenezaji wa DNA/RNA
7. Humkinga mama Mjamzito kupata Mimba Njiti na Mimba Kutoka
8. Kuimarisha na kuipa afya mifupa na Ngozi
9. Inakinga dhidi ya Mishipa kujeruhika na kukamaa sababu ya Mrundikano wa lehemu kwenye kuta za mishipa
10. Inakukinga dhidi ya Moyo Kupanuka-Metallothionine.
11. Inakinga mtu asipate madhara makubwa ya Pombe kwenye Ini, Madhara ya Mionzi na Dawa za Kansa.
12. Huimarisha usingizi, amani na Utulivu wa Ubongo, Kumbukumbu na Uwezo wa Kuelewa haraka (Melatonin na Serotonin)
13. Utendaji kazi mzuri wa tezi ya shingo, Thyroid gland. Zinc husaidia T3 receptor ifanye kazi, Unapopungukiwa unajihatarisha kupata Hypothyroidism.
14. Nywele kukatika na Kupotea kwa haraka
15. Husaidia matumizi ya sukari katika seli na uzalishaji wa insulin.

Asilimia 25-40 ya jamii duniani wana kabiliwa na upungufu wa madini ya zinc. Hasa hasa Nchi zenye uchumi wa kati na Chini zinakabiliwa sana na Tatizo hili.

Vyanzo vizuri vya Madini ya zinc ni Pamoja na Chaza, Pweza, Maini, Nyama Nyekundu, almonds mbegu za maboga nk. Tafiti zina onesha kwamba wale ambao hawali nyama nyekundu na vyakula vingine nilivyotaja hapo (Vegan) wako hatarini sana Kupungukiwa Madini ya Zinc. Pia watu wenye vidonda vya tumbo wanatumia dawa za kupunguza asidi, Wenye magonjwa ya Kuharisha muda mrefu, Wenye Magonjwa ya Ini na Figo wako hatarini sana kupungukiwa na madini ya zinc.
Kama ulaji wako ni mzuri unapanga sahani kwa usahihi. Ni vigumu sana Kupungukiwa madini haya. Lakini kama afya yako inakabiliwa na magonjwa kila leo na Ulaji wako sio sahihi Utahitaji Virutubisho sambamba na kuboresha sahani yako. Sio salama kiafya kutumia Virutubisho vyenye dozi kubwa kwa muda mrefu zaidi ya 100mg kwa siku. Hadi upate ushauri wa daktari.

Sawa ni Virutubisho lakini Fuata ushauri wa Kitalamu uwe na afya njema zaidi.

FUATILIA MAKALA YANGU IJAYO NITAFUNDISHA VYAKULA VYENYE UTAJIRI MKUBWA WA MADINI YA ZINC NA NAMNA YA KUVITUMIA.

Jiunga na Mafunzo ya Kupunguza uzito kupitia NHCP WEIGHTLOSS BOOTCAMP

Bonyeza link hapa kujifunza: http://nsambohealthcare.co.tz/weightlossbootcamp

0767 030 160

Duka la bidhaa za chakula na Mafunzo: nsamboshop.co.tz

Post a comment

Your email address will not be published.

18 − 4 =

Select the fields to be shown. Others will be hidden. Drag and drop to rearrange the order.
  • Image
  • SKU
  • Rating
  • Price
  • Stock
  • Availability
  • Add to cart
  • Description
  • Content
  • Weight
  • Dimensions
  • Additional information
Click outside to hide the comparison bar
Compare